Ushauri wa kibiashara kwa wafanyakazi na watu binafsi

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni  ya K-FINANCE inayotoa Mikopo na Ushauri wa Kibiashara kwa wafanyabiashara na watu binafsi Judith Minzi (aliyesimama), akipewa maelezo na moja ya washiriki wa maonyesho ya wanawake wajasiriamali maarufu kama Women in Business Balance Expo ya mwaka huu ambayo yalifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni. K-Finance ilidhamini maonyesho hayo kuongea na washiriki juu ya uhuru wa kiuchumi na vile vile kuhamasisha semina maarufu kama Ignite Business Clinic (IBC) Msimu wa pili ambayo ilifanyika Hekima Garden.