Walengwa
Wafanyabiashara wa kati na wakubwa katika maeneo ya Dar-es-Salaam na Dodoma
Viwango vya Mkopo
TZS 5M – TZS 50M
Lengo la Mkopo
Pesa ya kuendesha biashara kununua malighafi na mahitaji mengine ya kuendesha na kukuza biashara.
Muda wa Mkopo
Sio zaidi ya Miezi 6
Rejesho
Kila mwezi
Dhamana na Gharama za mkopo
- Usajili wa mkopo
- Gari iliyopo katika ubora unaoridhisha na ina bima kubwa.
- Tunakopea 3rd party dhamana kutoka kwa mdhamini wako pia.
- Nyumba/kiwanja kilicho endelezwa na zenye hati rasmi au leseni ya Makazi (mortgage itafanyika).
- Ada ya kuratibu mkopo ni 3% inayolipwa wakati wa kuchukua mkopo
- Ufungaji wa Car Track
Viambatanisho kwenye maombi ya mkopo
- Fomu ya ombi la mkopo lililojazwa kikamilifu
- Kitambulisho (copy ya kitambulisho cha uraia, kura, passport au udereva)
- Barua ya utambulisho wa serikali ya mtaa (nyumbani na biashara)
- Idhini ya Mwenzi wa ndoa (ambatanisha cheti cha ndoa au kiapo (AFFIDAVIT) kama huna ndoa
- Mkataba wa udhamini (Endapo Mkopaji hana makazi ya Kudumu Dar au Dodoma, ni sharti adhaminiwe na mtu mwenye makazi ya kudumu, ambatanisha bili za maji au umeme)
- Uthibitisho wa eneo la Biashara (Mkataba wa kupanga au uthibitisho wa umiliki (bill za maji au umeme)
- Uthibitisho wa uzoefu wa biashara usiopungua miezi 12 (Leseni ya Biashara, TIN namba au Tax Clearance, bank statement isiyopungua miezi 6)
- Taarifa ya mapato na matumizi zinazoonyesha historia ya biashara
- Uthibitisho wa mapato mengine ikiwa kama yapo
- Mkataba wa mradi