IBC 2020

Katika maktaba, mafunzo ya pili (module 2) ya IBC yaliyofanyika tarehe 18.01.2020 pale Hekima Garden na mkufunzi Bi Devotha Minzi ambae pia ni Mwanzilishi wa K-Finance. Mafunzo ya pili (module 2) yalijikita katika mbinu za kutambua vipaji vyako (potentials) na kuvitumia kuchagua kazi/biashara sahihi kwako kukufikisha kwenye uhuru wa kiuchumi. Mgeni Rasmi alikuwaKatibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezesahi Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa

Mafunzo ya Ignite Business Clinics kwa kifupi IBC, ni mafunzo maalumu na ya kipekee sana ambayo yamelenga katika kutoa elimu ya kufungua/kuamsha fikra za watu ili kujipatia uhuru endelevu wa kiuchumi. Tofauti na mafunzo mengi yanayotolewa; mafunzo ya IBC yamejitofautisha kwa kulenga katika mabadiliko ya kifikra (mindset change), ikizingatiwa kuwa tafiti nyingi zimeonyesha kuwa fikra na mitazamo hasi na uelewa finyu katika maswala ya kipesa, kazi na utafutaji mali kwa ujumla wake umekuwa tatizo kubwa sana katika jamii yetu