Ignite Business Clinic Registrations

Mafunzo ya Ignite Business Clinics kwa kifupi IBC, ni mafunzo maalum na ya kipekee sana ambayo yamelenga katika kutoa elimu ya kufungua/kuamsha fikra za watu ili kujipatia uhuru endelevu wa kiuchumi. Tofauti na mafunzo mengi yanayotolewa; mafunzo ya IBC yamejitofautisha kwa kulenga katika mabadiliko ya kifikra (mindset change), ikizingatiwa kuwa tafiti nyingi zimeonyesha kuwa fikra na mitazamo hasi na uelewa finyu katika maswala ya kipesa, kazi na utafutaji mali kwa ujumla wake umekuwa tatizo kubwa sana katika jamii yetu, husasani kwa Wanawake.
Mafunzo ya IBC, yatatolewa na watoa mada wazoefu katika maswala ya fedha na uendeshaji wa biashara. Mafunzo yatafanyika tarehe 18 January 2020. Yatakuwa ni mafunzo ya pili (Module 2) yakifuatiwa na mafunzo ya kwanza yaliyozinduliwa tarehe 19 October 2019. Mafunzo ya pili (module 2) yatajikita katika mbinu za kutambua vipaji vyako (potentials) na kuvitumia kuchagua kazi/biashara sahihi kwako kukufikisha kwenye uhuru wa kiuchumi.

Katika module hii ya pili ya tarehe 18 January 2020, tutakusaidia mlengwa kujihoji na kutafakari kwa kina jinsi ya kutambua vipaji vyake na kuchukua hatua kujifanyia mabadiliko ili kufikia uhuru wa kiuchumi. Mada hii ni muhimu sana kwa kila mtu na hata kwa wazazi. Chimbuko la mada hii ni uhitaji wa soko. Kuna uhitaji mkubwa wa watu kujitambua na kujua wafanye biashara gani. Mara tumesikia watu wakisema wanatamani kufanya biashara ila hawajui wafanye biashara gani. Wengi wamekimbilia kusema kuwa tatizo ni mtaji. Lakini je utatafutaje mtaji wakati hujui cha kufanya? Ni muhimu sana mtu kujitambua wewe ni nani na una nini tayari mezani kama mtaji wako kuelekea kwenye uhuru wa kiuchumi. Tutaangalia namna ya kuoanisha vipaji/potential na fursa zilizopo sokoni. Ikumbukwe hapa mtaji sio pesa pekee, ni vyote ulivonavyo pamoja na elimu, mtandao wako, tabia yako na mitazamo yako chanya katika maswala mbalimbali. Vilevile, tutajifunza namna ya kujenga/kukuza vipaji vyako.

Nini chimbuko la mafunzo ya IBC?
Akielezea kwa hisia, Mama Devotha Minzi ambaye ni mkufunzi mkuu na muanzilishi wa IBC program anasema, “Mafunzo ya IBC, yamebeba ujuzi na uzoefu wangu wa karibia miaka 60 ya maisha yangu. Mimi kwa taaluma ni mchumi; nimefanya kazi na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa zaidi ya miaka 20. Nikisukumwa na wazo la kujipatia uhuru endelevu wa kiuchumi, kwa mshangao mkubwa wa wengi, niliacha kazi BOT (dream employer to many) nikiwa na umri wa miaka 48 tu na kwenda kuanzisha kampuni ya K-Finance LTD.”

Mama Devotha-Mwenyekiti wa Board ya Wakurugenzi ya K-Finance LTD. Akiwa muanzilishi na Mkurugenzi wa kwanza wa K-Finance LTD. Kampuni yenye uzoefu wa zaidi ya miaka kumi katika huduma za kifedha, hususani kwa wajasiriamali. K-Finance LTD inajihusisha pia katika kutoa mafunzo na ushauri katika maswala ya fedha na kibiashara. Kitaaluma mama Minzi ni mchumi akiwa na degree ya pili katika uchumi. Pia ni ‘certified Director wa IoD –London’. Amepata elimu ya juu kuhusu mipango mikakati ya uongozi na usimamizi wa biashara. Vilevile, amepata bahati ya kuwa mkurugenzi katika bodi za makampuni na taasisi mbalimbali. Kutokana na uzoefu wake, Mama Devotha ametambua na kugundua kuwa jamii ya kitanzania ina changamoto kubwa ya kifikra (mindset) juu ya namna ya kuzitambua fursa na kuzifanyia kazi ili kupata mafanikio endelevu ya kiuchumi. Na hivyo basi, mafunzo ya IBC yanalenga kuchangia katika kuziba pengo hilo na kuweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi.

Taarifa muhimu:
Siku: Jumamosi, Tar 18/01/2020
Mahali: Hekima Gardens – Mikocheni
Muda: Saa 3:00 Asubuhi – Saa 7:00 Mchana

Link ya Fomu ya Usajili: https://forms.gle/a5f1JZFiZz7aqg7V9